Posts

YAJUE KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU ILI KULETA THAMANI KWENYE MAISHA YAKO

Image
  …UTAIINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI… (Isaya 58:12) Mafundisho ya Neno la Mungu  Na: Isaac Mwanzalila  Mtu aliumbwa ili kulitenda kusudi la Mungu katika maisha yake, naam kusudi ambalo limebeba mapenzi ya Mungu. Kadri mtu anavyoyatenda mapenzi ya Mungu ndivyo anavyozidi kuongezeka kiufahamu katika kulitumikia kusudi la Mungu. Kimsingi maisha ya mtu hayana thamani kama ataishi nje ya mapenzi ya Mungu akali hapa duniani. Pale tu anapoishi kwa kuyatenda mapenzi ya Mungu ndipo anapoleta thamani au maana halisi ya maisha yake hapa duniani. Yeremia 29:11 ‘Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho’.   Tambua kwamba mawazo ya Mungu yanatuonyesha mapenzi yake kwetu na hivyo mawazo yake ndiyo mapenzi yake kwetu. Si watu wengi wanaojua kwamba kutokuyatenda mapenzi ya Mungu ni dhambi.  Yakobo 4:17 ‘Bali yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi’.  Ndio yeye m...

YATAZAME MAMBO KUTOKA KWENYE ULIMWENGU WA KIROHO ILI UFANIKIWE

Image
... UTAINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI...(ISAIAH 58:12)  …UTAIINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI… (Isaya 58:12) Mafundisho ya Neno la Mungu …UTAIINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI… (Isaya 58:12) Mafundisho ya Neno la Mungu Na: Isaac Mwanzalila   Katika 2 Wafalme 6:15-17 imeandikwa ‘ Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje? Akamjibu, USIOGOPE; maana WALIO PAMOJA NASI ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote’. Kuna tofauti kubwa sana ya kuyatazama mambo kwa macho ya mwili na kuyatazama kwa macho ya kiroho. Ndio, ipo tofauti ya kuona mambo kutokea kwenye ufalme wa nuru na kuyaona kutokea kwenye ufalme wa ...

SHULE YA MUNGU MAISHANI MWAKO.

Image
... UTAINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI...(ISAYA 58:12) Na: Isaac Mwanzalila   KWELI_KUU: Maisha ni uanafunzi katika kujifunza kumjua Mungu kwa kumjua Kristo Yesu Bwana. Zaburi 32:8 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea, Nitakushauri, jicho langu likikutazama UTANGULIZI Shule ni muunganiko wa madarasa tofauti tofauti katika ngazi na viwango tofauti tofauti yenye lengo la kumfundisha mtu mtu kujua jambo, au mambo fulani au kitu fulani kwa kina na weledi sana. Na katika shule kuna vipimo au mitiani toka darasa hadi darasa ambavyo hutumika kumpima mtu kama amejua na kufahamu jambo fulani na kwamba anastahili kuvuka na kwenda ngazi au kiwango cha juu zaidi kwa kuingia darasa linalofundisha viwango hivyo vya elimu au mafundisho. Lengo ni mwanafunzi afikie kiwango fulani cha kujua jambo fulani kitakachomsaidia kuishi maisha yake kwa ufahamu na ujuzi aliona juu ya jambo lile akikabiliana na changamoto za kimaisha anazokuta nazo siku kwa siku. Mungu anayoshule katika maisha yetu, na...

KIJANA AU BINTI USIJIDANGANYE KWENYE NDOA HUTAISHI NA UMBILE WALA FEDHA

Image
  …UTAIINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI… (Isaya 58:12) Mafundisho ya Neno la Mungu  Na: Isaac Mwanzalila  Mwaka fulani nikiwa chuo mwalimi mmoja aliniambia, Isaac ukitaka kuoa tafuta binti mwenye sura na umbile zuri ambaye kila atakayekuona naye atasema kwa kweli mwenzetu Isaac kapata mke. Nikiwa mkoa mwingine kimasomo Mzee mmoja wa kanisa aliniambia jambo la aina hiyo pia. Naam si hawa tu waliojaribu kunijengea wazo la aina hii, wapo na wengine, ila nimeamua kutaja hawa wawili kutokana na nafasi zao kama viongozi. Hata leo vijana wengi katika kutafuta mwenza wa maisha wanaongozwa na matakwa yao binafsi ambayo mengi ni kinyume na mapenzi ya Mungu kwenye maisha yao. Ukweli ni kwamba wanaume wengi huangalia muonekano wa nje wa mwanamke hususani sura, rangi na umbile lake, hii ni kwa sababu wanaume wengi wanaamini zaidi katika mvuto na muonekano wa nje wa mwenza. Upande wa pili wadada wengi licha ya kujali pia suala la muonekano wa nje, wao huangalia zaidi uwezo wa mtu kifedha n...

MAMBO YA KUMSAIDIA KIJANA ALIYEOKOKA AISHI MAISHA YENYE USHUHUDA MZURI

Image
…UTAIINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI… (Isaya 58:12)  Mafundisho ya Neno la Mungu  Na: Isaac Mwanzalila  Mtume Paulo katika waraka wake kwa Timotheo anamwambia hivi, ‘Mtu awaye yote ASIUDHARAU ujana wako, bali uwe KIELELEZO kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. JITUNZE nafsi yako, na mafundisho yako. DUMU katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo UTAJIOKOA NAFSI YAKO NA WALE WAKUSIKIAO PIA’ (1Timotheo 4:12 & 14). Sentensi hizi zinatuonyesha kwamba kijana yeyote ambaye amefanya uamuzi wa kuokoka, kwa hakika amefanya maamuzi ambayo yanamtaka amaanishe katika kumfuata kwake Yesu au kuuishi wakovu wake. Pamoja na kumpa Yesu maisha yake ni lazima kijana afanye maamuzi ya kuishi maisha ya kudumu kumpendeza Mungu kwa kuzikubali gharama zinazohusiana na wokovu aliouchagua na si kuishi maisha yenye kupelekea jina la BWANA kutukanwa kama ilivyo kwa baadhi ya vijana wengi leo. Ukisoma mstari huu wa 1Timotheo 4:14 kwenye toleo la kiingere...