YAJUE KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU ILI KULETA THAMANI KWENYE MAISHA YAKO

…UTAIINUA MISINGI YA VIZAZI VINGI… (Isaya 58:12) Mafundisho ya Neno la Mungu Na: Isaac Mwanzalila Mtu aliumbwa ili kulitenda kusudi la Mungu katika maisha yake, naam kusudi ambalo limebeba mapenzi ya Mungu. Kadri mtu anavyoyatenda mapenzi ya Mungu ndivyo anavyozidi kuongezeka kiufahamu katika kulitumikia kusudi la Mungu. Kimsingi maisha ya mtu hayana thamani kama ataishi nje ya mapenzi ya Mungu akali hapa duniani. Pale tu anapoishi kwa kuyatenda mapenzi ya Mungu ndipo anapoleta thamani au maana halisi ya maisha yake hapa duniani. Yeremia 29:11 ‘Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho’. Tambua kwamba mawazo ya Mungu yanatuonyesha mapenzi yake kwetu na hivyo mawazo yake ndiyo mapenzi yake kwetu. Si watu wengi wanaojua kwamba kutokuyatenda mapenzi ya Mungu ni dhambi. Yakobo 4:17 ‘Bali yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi’. Ndio yeye m...